Taarifa ya Marekebisho ya Awamu ya Sita ya Takwimu za Pato la Taifa Mwaka wa Kizio 2015

Pato la Taifa la mwaka 2015 kwa bei za miaka husika kizio cha mwaka 2015 lilikuwa shilingi za Tanzania Trilioni 94.3 ikilinganishwa na Pato la Taifa la mwaka 2015 kwa bei za miaka husika kizio cha mwaka 2007 lilikuwa shilingi za Tanzania Trilioni 90.8.

Katika mwaka wa kizio wa 2015, mchango wa shughuli za kiuchumi za Kilimo, Misitu na Uvuvi katika la Pato la Taifa ulikuwa asilimia 25.1 mwaka 2017 ukilinganishwa na asilimia 24.86 mwaka 2016. Hata hivyo, mchango wa shughuli za Viwanda na Ujenzi pamoja na Huduma ziliongezeka kwa asilimia 24.5 na 40.4 kwa mwaka wa kizio 2015 ukilinganisha na asilimia 24.0 na 39.5 kwa mwaka wa kizio 2007 kwa mfuatano huo.

Mwaka 2018, takwimu za Pato la Taifa kwa Robo mwaka zilizorekebishwa kizio cha 2015 zinaonesha kuwa kasi kubwa ya ukuaji ya asilimia 7.1 ilikuwa katika Robo ya Kwanza wakati kasi ndogo katika kipindi hicho ya asilimia 6.3 ilikuwa katika Robo ya Pili. Hata hivyo, wastani wa kasi ya ukuaji katika kipindi cha Januari hadi Septemba, 2018 ilikuwa asilimia 6.8. Kasi ya ukuaji katika robo ya Nne mwaka 2018 itapatikana katika Taarifa ya Pato la Taifa kwa Robo Mwaka inayotarajiwa kutolewa mwishoni mwa mwezi Machi 2019.

Bonyeza hapa kwa taarifa zaidi