Pato la Taifa katika kipindi cha robo ya Kwanza (Januari - Machi) ya mwaka 2021, katika bei za miaka husika liliongezeka hadi shilingi trilioni 38.0 kutoka shilingi trilioni 36.4 kipindi kama hicho mwaka 2020. Aidha, katika kipindi hicho, Pato la Taifa kwa bei za mwaka 2015 liliongezeka hadi shilingi trilioni 33.2 kutoka shilingi trilioni 31.7 katika kipindi kama hicho mwaka 2020 sawa na ukuaji wa asilimia 4.9.

Bonyeza hapa kupakua ripoti nzima