Pato la Taifa katika kipindi cha Robo ya Pili (Aprili - Juni) ya mwaka 2021, kwa bei za miaka husika liliongezeka hadi shilingi trilioni 39.2 kutoka shilingi trilioni 37.2 kipindi kama hicho mwaka 2020. Aidha, katika kipindi hicho, Pato Halisi la Taifa liliongezeka hadi shilingi trilioni 33.4 kutoka shilingi trilioni 32.0 katika kipindi kama hicho mwaka 2020 sawa na ukuaji wa asilimia 4.3.

Bonyeza hapa kupakua ripoti nzima