CPI December 2013 

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Desemba, 2013 umepungua hadi asilimia 5.6 kutoka asilimia 6.2 mwezi Novemba, 2013.

Kupungua kwa Mfumuko wa Bei wa mwezi Desemba, 2013 kunamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwezi Desemba, 2013 imepungua ikilinganishwa na kasi ya kupanda kwa bei kwa mwezi Novemba, 2013.

Aidha, Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 144.07 kwa mwezi wa Desemba, 2013 kutoka 136.48 mwezi Desemba, 2012. Mfumuko wa Bei wa Vyakula na Vinywaji Baridi umepungua hadi asilimia 6.0 mwezi Desemba, 2013 kutoka asilimia 7.2 ilivyokuwa mwezi Novemba, 2013.

Click here to open Full Details in Pdf format...