Maandalizi ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016

Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI (THIS) wa mwaka 2016 ni Utafiti wa kitaifa unaotumia sampuli kutoa taarifa zinazohusiana na watu, maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI (VVU), kupunguza kiasi cha VVU mwilini (viral load suppression), kuenea kwa maambukizi ya VVU, Idadi ya chembechembe za kinga mwilini (CD4), tabia hatarishi zinazopelekea maambukizi ya VVU, kiwango cha maambukizi ya VVU kwa watoto na   utumiaji wa huduma zinazohusiana na VVU kama vile kinga na tiba. Utafiti huu utahusisha mahojiano na watu wenye umri wa miaka 15 na zaidi. Wahojiwa wataulizwa maswali kuhusu taarifa zao binafsi, hali ya ndoa, uzazi na taarifa za afya za watoto wao wenye umri chini ya miaka 14, tohara ya wanaume, uelewa na mtazamo wao kuhusiana na VVU, Hali ya VVU na taarifa nyingine ambazo zitawasaidia watunga sera na watawala kwenye programu za Afya na VVU. Utafiti huu pia utawahoji vijana wa rika-balehe wenye umri kati ya miaka 10-14, juu ya taarifa zao binafsi, uelewa na ufahamu juu ya masuala na programu za VVU, tabia zao katika kujamiiana na upimaji wa VVU.

Kuna aina aina tatu za madodoso yatakayotumika kukusanya taarifa katika utafiti huu, ambayo ni:-

Ukiwa Mdau wa utafiti huu, tunaomba utume maoni yako kwenye barua pepe ifuatayo:

Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Mwisho wa kupokea maoni ni tarehe 15 Juni, 2016