• takwimuhouse

    Mchoro wa jengo jipya la "TAKWIMU HOUSE" linaloendelea kujengwa mjini Dodoma. Jengo hili ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Kabambe wa kuboresha Takwimu Tanzania (TSMP)

Kanzadata ya Takwimu za Watu wenye Ulemavu

Takwimu zilizomo katika kanzadata ni pamoja na takwimu za kidemografia na hali ya uchumi. Takwimu hizi zinasaidia watunga sera, vyama vya watu wenye ulemavu, waandishi wa habari, na umma kujua changamoto zilizopo na kuchukua hatua. Takwimu zinazopatikana katika Kanzadata hii ni pamoja na taarifa juu ya idadi ya watu wenye ulemavu ikihusianishwa na hali zao za ajira, elimu, kipato cha kaya binafsi, hali ya umaskini , nk.

Takwimu zimetokana na Tafiti zifuatazo;-

  • Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi (ILFS 2014)
  • Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi (HBS 2011/2012)
  • Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 (PHC 2012)
  • Utafiti wa Kufuatilia Umaskini Tanzania (NPS 2010/2011)
  • Utafiti wa Watu Wenye Ulemavu (DISABILITY SURVEY 2008)
  • Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2002(PHC 2002)

ulemavu 8113f

Takwimu za Leo

Mfumuko wa Bei

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Septemba, 2017 umeongezeka hadi asilimia 5.3 kutoka asilimia 5.0 mwezi Agosti, 2017. 

Kwa taarifa kamili bonyeza hapa