Kitabu Cha Hali Ya Uchumi 2013

Mwaka 2013, Pato halisi la Taifa lilikua kwa kiwango cha asilimia 7.0 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 6.9 mwaka 2012.

Ukuaji huu ulitokana na kuimarika kwa sekta zinazochangia Pato la Taifa kwa kiasi kikubwa hususan sekta za kilimo, ujenzi na biashara. Ukuaji wa viwango vya juu ulijionesha katika shughuli ndogo za kiuchumi za: mawasiliano (asilimia 22.8); fedha (asilimia 12.2); ujenzi (asilimia 8.6); na biashara (asilimia 8.3).

Pamoja na kuwa na viwango vikubwa vya ukuaji, sekta za mawasiliano na fedha bado zinachangia kiwango kidogo katika Pato la Taifa cha chini ya wastani wa asilimia 2.5.

Bonyeza HAPA kupata Kitabu chenye taarifa kamili ya Hali ya Uchumi kwa mwaka 2013 .....   (Ukubwa wa file ni 3.2Mb)