Kitabu cha Hali ya Uchumi kwa Mwaka 2014

Serikali kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu ilifanya marekebisho ya takwimu za Pato la Taifa kwa kutumia mwaka 2007 kuwa mwaka wa kizio kutoka mwaka wa kizio wa 2001.

Mwaka 2007 umetumika kwa vile ulikuwa na taarifa nyingi kutoka vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na tafiti za kiuchumi, kijamii na taarifa za kiutawala. Umuhimu wa marekebisho hayo unatokana na maendeleo ya kiuchumi na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

Mabadiliko hayo yamesababisha kuwepo kwa haja ya kufanya marekebisho na kujumuisha thamani ya bidhaa na huduma mpya katika Pato la Taifa ambazo hapo awali hazikuwepo - mfano gesi asilia, sanaa na burudani na huduma za fedha kupitia mitandao ya simu za kiganjani.

Maelezo ya kina kuhusu marekebisho hayo yako katika sura ya kumi. Hivyo, kuanzia mwaka huu, takwimu zitakazotumika zitakuwa za mwaka wa kizio wa 2007.

Kwa mujibu wa takwimu mpya za mwaka wa kizio wa 2007, Pato halisi la Taifa lilikua kwa kiwango cha asilimia 7.0 mwaka 2014 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 7.3 mwaka 2013.

Bonyeza HAPA kupata Kitabu chenye taarifa kamili ya Hali ya Uchumi kwa mwaka 2014 ....... (Ukubwa wa file ni 2Mb)