Taarifa Kuhusu Pato La Taifa Kwa Robo ya Kwanza ya Mwaka (Januari – Machi, 2015)

Ofisi ya Taifa ya Takwimu ina jukumu la kutayarisha na kusambaza takwimu rasmi nchini ikiwa ni pamoja na takwimu za Pato la Taifa kwa robo Mwaka. Takwimu za Pato la Taifa kwa robo mwaka hupimwa kwa kuangalia thamani ya bidhaa na huduma zilizozalishwa nchini katika vipindi vya miezi mitatu mitatu. Utayarishaji wa Takwimu za Pato la Taifa hujumuisha shughuli zote za kiuchumi na hivyo hutumika katika kutathmini, kupanga mipango na kutayarisha sera za kiuchumi.

Takwimu za robo mwaka ya kwanza zilizowasilishwa tarehe 13 Agosti 2015 (Januari – Machi) kwa bei za miaka inayohusika na mwaka wa 2007 zinasambazwa kwa mara ya tatu ambazo zimetayarishwa kwa kuzingatia marekebisho ya Takwimu za Pato la Taifa kwa bei za mwaka 2007.

Thamani ya Pato la Taifa kwa robo ya kwanza ya mwaka 2015 kwa bei za mwaka 2007 imeongezeka na kufikia TZS 10.6 trilioni kutoka TZS 9.9 trilioni zilizopatikana katika kipindi kama hicho mwaka 2014 ikiwa ni sawa na ukuaji wa asilimia 6.5 kwa mwaka 2015 ikilinganishwa na asilimia 8.6 ya ukuaji kipindi kama hicho mwaka 2014.

Matokeo ya takwimu za Pato la Taifa kwa robo mwaka kwa bei za miaka inayohusika yameonyesha kuwa thamani ya Pato la Taifa katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2015 ilikuwa TZS 21.9 trilioni ikilinganishwa na TZS 18.6 trilioni zilizopatikana kipindi kama hicho mwaka 2014.

Bonyeza hapa kupata Taarifa zaidi ...