Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Septemba, 2015 umepungua hadi asilimia 6.1 kutoka asilimia 6.4 ilivyokuwa mwezi Agosti, 2015.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2015 imepungua ikilinganishwa

na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2015. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 159.04 kwa mwezi Septemba, 2015

kutoka 149.93 mwezi Septemba, 2014. Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwezi Septemba, 2015 umepungua

hadi asilimia 9.6 kutoka asilimia 10.2 ilivyokuwa mwezi Agosti, 2015.

Pata taarifa kamili hapa...