CPI Agosti 2015 (Kiswahili)

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Agosti, 2015 umebaki kuwa asilimia 6.4 kama ilivyokuwa mwezi Julai, 2015.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2015 imekuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2015. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 158.81 kwa mwezi Agosti, 2015 kutoka 149.31 mwezi Agosti, 2014.

Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwezi Agosti, 2015 umepungua hadi asilimia 10.2 kutoka asilimia 10.6 ilivyokuwa mwezi Julai, 2015.

Pata taarifa kamili hapa...