CPI Juni 2015 (Kiswahili)

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Juni, 2015 umeongezeka hadi asilimia 6.1 kutoka asilimia 5.3 ilivyokuwa mwezi Mei, 2015.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2015 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2015.

Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 158.12 kwa mwezi Juni, 2015 kutoka 148.98 mwezi June, 2014. Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwezi Juni, 2015 umeongezeka hadi asilimia 10.1 kutoka asilimia 8.5 ilivyokuwa mwezi Mei, 2015.

Pata taarifa kamili hapa...