CPI Mei 2015 (Kiswahili)

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Mei, 2015 umeongezeka hadi asilimia 5.3 kutoka asilimia 4.5 ilivyokuwa mwezi Aprili, 2015.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2015 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili, 2015. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 157.86 kwa mwezi Mei, 2015 kutoka 149.89 mwezi Mei, 2014. Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwezi Mei, 2015 umeongezeka hadi asilimia 8.5 kutoka asilimia 7.1 ilivyokuwa mwezi Aprili, 2015.

Pata taarifa kamili hapa...