CPI Machi 2015 (Kiswahili)

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Machi, 2015 umeongezeka kidogo hadi asilimia 4.3 kutoka asilimia 4.2 ilivyokuwa mwezi Februari, 2015.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Machi, 2015 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2015.

Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 155.88 kwa mwezi Machi, 2015 kutoka 149.49 mwezi Machi, 2014. Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwezi Machi, 2015 umeongezeka hadi asilimia 5.9 kutoka asilimia 4.9 ilivyokuwa mwezi Februari, 2015.

Pata taarifa kamili hapa...