CPI Desemba 2014 (Kiswahili)

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Desemba, 2014 umepungua hadi asilimia 4.8 kutoka asilimia 5.8 ilivyokuwa mwezi Novemba, 2014.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba, 2014 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2014.

Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 150.92 kwa mwezi Desemba, 2014 kutoka 144.07 mwezi Desemba, 2013. Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi umepungua hadi asilimia 5.7 mwezi Desemba 2014 kutoka asilimia 7.0 mwezi Novemba, 2014.

Kwa taarifa kamili endelea hapa