CPI Agosti 2014 (Kiswahili)

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Agosti, 2014 umeongezeka hadi asilimia 6.7 kutoka asilimia 6.5 ilivyokuwa mwezi Julai, 2014.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2014 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2014. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 149.31kwa mwezi wa Agosti, 2014 kutoka 139.93 mwezi Agosti, 2013.

Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi umeongezeka hadi asilimia 8.8 mwezi Agosti 2014 kutoka asilimia 8.1 ilivyokuwa mwezi Julai, 2014.

Kwa taarifa kamili endelea hapa