CPI Julai 2014 (Kiswahili)

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Julai, 2014 umeongezeka kidogo hadi asilimia 6.5 kutoka asilimia 6.4 ilivyokuwa mwezi Juni, 2014.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2014 imeongezeka kidogo ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2014. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 149.16kwa mwezi wa Julai, 2014 kutoka 140.01 mwezi Julai, 2013. Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi umebaki kuwa asilimia 8.1 mwezi Julai 2014 kama ilivyokuwa mwezi Juni, 2014.


Kwa taarifa kamili endelea hapa