CPI Juni 2014 (Kiswahili)

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Juni, 2014 umepungua hadi asilimia 6.4 kutoka asilimia 6.5 ilivyokuwa mwezi Mei, 2014.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2014 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2014.

Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 148.98 kwa mwezi wa Juni, 2014 kutoka 140.00 mwezi Juni, 2013. Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi umepungua hadi asilimia 8.1 mwezi Juni, 2014 kutoka asilimia 8.7 ilivyokuwa mwezi Mei, 2014.

Kwa taarifa kamili endelea hapa .