CPI Mei 2014 (Kiswahili)

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Mei, 2014 umeongezeka hadi asilimia 6.5 kutoka asilimia 6.3 ilivyokuwa mwezi Aprili, 2014.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2014 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili, 2014.

Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 149.89 kwa mwezi wa Mei, 2014 kutoka 140.76 mwezi Mei, 2013. Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi umeongezeka hadi asilimia 8.5 mwezi Mei, 2014 kutoka asilimia 7.8 ilivyokuwa mwezi Aprili, 2014.

Kwa taarifa kamili endelea hapa ....