CPI Aprili 2014 (Kiswahili)

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Aprili, 2014 umeongezeka hadi asilimia 6.3 kutoka asilimia 6.1 ilivyokuwa mwezi Machi, 2014. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwezi Aprili, 2014 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo mwezi Machi, 2014.

Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 150.50 kwa mwezi wa Aprili, 2014 kutoka 141.59 mwezi Aprili, 2013. Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi umeongezeka hadi asilimia 7.8 mwezi Aprili, 2014 kutoka asilimia 7.2 ilivyokuwa mwezi Machi, 2014.

Kwa taarifa kamili endelea hapa ....