CPI Machi 2014 (Kiswahili)

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Machi, 2014 umeongezeka kidogo hadi asilimia 6.1 kutoka asilimia 6.0 ilivyokuwa mwezi Februari, 2014. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwezi Machi, 2014 imeongezeka kidogo ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo mwezi Februari, 2014.

Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 149.49 kwa mwezi wa Machi, 2014 kutoka 140.93 mwezi Machi, 2013. Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi umeongezeka hadi asilimia 7.2 mwezi Machi, 2014 kutoka asilimia 6.2 mwezi Februari, 2014.

Kwa taarifa kamili endelea hapa ....