CPI Februari 2014 (Kiswahili)

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha badiliko la kasi ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Februari, 2014 umebakia kuwa asilimia 6.0 kama ilivyokuwa mwezi Januari, 2014.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwezi Februari, 2014 imebakia kuwa sawa na kasi iliyokuwepo mwezi Januari, 2014. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 148.62 kwa mwezi wa Februari, 2014 kutoka 140.23 mwezi Februari, 2013. Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi umeongezeka hadi asilimia 6.2 mwezi Februari, 2014 kutoka asilimia 6.0 mwezi Januari, 2014.

Kwa taarifa kamili endelea hapa ....