Mfumuko wa Bei Januari 2016

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Januari, 2016 umepungua hadi asilimia 6.5 kutoka asilimia 6.8 ilivyokuwa mwezi Desemba, 2015.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2016 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba, 2015.

Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 100.71 kwa mwezi Januari, 2016 kutoka 94.54 ambazo ni Fahirisi za mwezi Januari, 2015 zilizofanyiwa marejeo. Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwezi Januari, 2016 umepungua kidogo hadi asilimia 10.7 kutoka asilimia 11.1 ilivyokuwa mwezi Desemba, 2015.

Pata taarifa kamili hapa...