Mfumuko wa Bei February 2016

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Februari, 2016 umepungua hadi asilimia 5.6 kutoka asilimia 6.5 ilivyokuwa mwezi Januari, 2016.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2016 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2016.

Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 101.44 kwa mwezi Februari, 2016 kutoka 96.03 ambazo ni Fahirisi za mwezi Februari, 2015 zilizofanyiwa marejeo. Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwezi Februari, 2016 umepungua hadi asilimia 9.5 kutoka asilimia 10.7 ilivyokuwa mwezi Januari, 2016. 

Pata taarifa kamili hapa...