Mfumuko wa Bei Machi 2016

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Machi, 2016 umepungua hadi asilimia 5.4 kutoka asilimia 5.6 ilivyokuwa mwezi Februari, 2016.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Machi, 2016 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2016.

Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 101.93 kwa mwezi Machi, 2016 kutoka 96.69 mwezi Machi, 2015. Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwezi Machi, 2016 umepungua kidogo hadi asilimia 8.3 kutoka asilimia 9.5 ilivyokuwa mwezi Februari, 2016.

Pata taarifa kamili hapa...