Mfumuko wa Bei Aprili 2016

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Aprili, 2016 umepungua hadi asilimia 5.1 kutoka asilimia 5.4 ilivyokuwa mwezi Machi, 2016.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili, 2016 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Machi, 2016.

Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 102.46 mwezi Aprili, 2016 kutoka 97.50 mwezi Aprili, 2015. Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi mwezi Aprili, 2016 umepungua kidogo hadi asilimia 7.1 kutoka asilimia 8.3 ilivyokuwa mwezi Machi, 2016.

Pata taarifa kamili hapa...