Mfumuko wa Bei mwezi Juni 2016

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Juni, 2016 umeongezeka hadi asilimia 5.5 kutoka asilimia 5.2 ilivyokuwa mwezi Mei, 2016. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2016 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2016. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 103.47 mwezi Juni, 2016 kutoka 98.10 mwezi Juni, 2015.

Pata taarifa kamili hapa...