Mfumuko wa Bei mwezi Julai 2016

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Julai, 2016 umepungua hadi asilimia 5.1 kutoka asilimia 5.5 ilivyokuwa mwezi Juni, 2016. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2016 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2016. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 103.50 mwezi Julai, 2016 kutoka 98.48 mwezi Julai, 2015. Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi mwezi Julai, 2016 umepungua hadi asilimia 7.6 kutoka asilimia 8.1 ilivyokuwa mwezi Juni, 2016.  

 Pata taarifa kamili hapa