Mfumuko wa Bei Novemba 2016

Mfumuko wa Bei Novemba 2016 Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Novemba, 2016 umeongezeka hadi kufikia asilimia 4.8 kutoka asilimia 4.5 mwezi Oktoba, 2016. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2016 imeongezeka ikilinganishwa na kasi ya upandaji ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2016. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 104.32 mwezi Novemba, 2016 kutoka 99.54 mwezi Novemba, 2015. Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwezi Novemba, 2016 umeongezeka hadi asilimia 6.2 kutoka asilimia 6.0 ilivyokuwa mwezi Oktoba, 2016.

Bonyeza hapa kupata mfumuko wa Bei wa mwezi Novemba