Mfumuko wa Bei kwa mwezi Machi 2017

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Machi, 2017 umeongezeka hadi kufikia asilimia 6.4 kutoka asilimia 5.5 mwezi Februari, 2017.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Machi, 2017 imeongezeka ikilinganishwa na kasi ya upandaji ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2017. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 108.44 mwezi Machi, 2017 kutoka 101.93 mwezi Machi, 2016. Mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwezi Machi, 2017 umeongezeka hadi asilimia 11.0 kutoka asilimia 8.7 ilivyokuwa mwezi Februari, 2017.

Kwa taarifa kamili bonyeza hapa