|
SENSA YA WATU NA MAKAZI NI MUHIMU KATIKA MIPANGO
YA MAENDELEO - “Jiandae Kuhesabiwa 26 Agosti 2012”
Historia ya Sensa Tanzania.
Sensa ya kwanza Tanzania ilifanyika mwaka 1910. Sensa nne za Mwisho zilifanyika baada ya Uhuru, katika miaka ya 1967, 1978, 1988 na 2002. Kulingana na sensa ya mwisho iliyofanyika mwezi Agosti 2002, idadi ya watu nchini Tanzania ilikuwa 34,443,603. |
|
|
Maelezo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu Sensa ya Majaribio ya Watu na Makazi ya Mwaka 2011.

Sensa ya majaribio ya watu na makazi imefanyika nchini Tanzania katika kaya 5,000. Sensa hiyo imefanyika kwenye maeneo 44 ya kuhesabia watu katika mikoa 11. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitoa maelezo kwa wananchi kuhusu Sensa ya Majaribio ya watu na makazi ya mwaka 2011. Bonyeza hapa kusoma Maelezo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
|
|
Maswali yaulizwayo mara kwa mara (Frequently Asked Questions)
Sensa ya Watu na Makazi ni nini?
Sensa ya Watu na Makazi ni utaratibu wa kupata na kurekodi habari kuhusu watu na makazi yao.
Bonyeza hapa kupata maswali na majibu zaidi.
|
|
|
MADODOSO YANAYOTUMIKA (Questionnaires.)
Kuna aina mbili ya madodoso yanayotumika katika Sensa ya Majaribio ya Watu na Makazi ya mwaka 2011. Kuna Dodoso-refu (long Questionnaire) na Dodoso-fupi (Short Questionnaire). Madodoso haya yametengenezwa kwa kutumia teknolojia ya OMR (Optical Mark Reader) lakini hapa yamewekwa kwenye mfumo wa excel ili kukuwezesha kuyasoma na kuyaelewa. Ukiwa na maoni ya uboreshaji usisite kuwasiliana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu.
|
| Tanzania:Matokeo ya Sensa ya Watu 1967-2002 na Makadirio kati ya mwaka 2003-2025 |
| Mwaka |
Idadi |
|
Mwaka |
Idadi |
| 1967 |
12,313,469 |
|
2006 |
38,250,927 |
| 1978 |
17,512,610 |
|
2009 |
41,915,880 |
| 1988 |
23,095,885 |
|
2010 |
43,187,823 |
| 2002 |
34,443,603 |
|
2012 |
45,798,475 |
| 2003 |
34,859,582 |
|
2015 |
49,861,768 |
| 2004 |
35,944,015 |
|
2020 |
57,102,896 |
| 2005 |
37,083,346 |
|
2025 |
65,337,918 |
|
|
|