Taarifa ya hali ya uhalifu ya kipindi cha Januari hadi Desemba, 2017 imeangalia kwa ujumla matukio mbalimbali ya uhalifu yaliyoripotiwa nchini katika kipindi hicho. Matukio yamegawanywa katika makundi mawili ambayo ni makosa makubwa na madogo ya jinai na ya usalama barabarani. Makosa ya jinai yamegawanywa katika makundi matatu; makosa dhidi ya binadamu, makosa ya kuwania mali na makosa dhidi ya maadili ya jamii.

Katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Desemba, 2017, jumla ya matukio 3,119,531 ya jinai na usalama barabarani yaliripotiwa katika vituo vya polisi nchini, yakilinganishwa na matukio 2,850,013 yaliyoripotiwa katika kipindi kama hicho cha mwaka 2016. Hili ni ongezeko la matukio 269,518 ambalo ni sawa na asilimia 9.5.

Click Here to Download the Crime Statistics Report Jan - Dec 2017 (PDF Format)

Click Here to Download the Crime Statistics Report Jan - Dec 2017 (Zip Format)