Taarifa ya hali ya uhalifu ya kipindi cha Januari hadi Desemba, 2019 imeangalia kwa ujumla matukio mbalimbali ya uhalifu yaliyoripotiwa katika vituo vya polisi nchini katika kipindi hicho. Matukio yamegawanywa katika makundi mawili ambayo ni makosa makubwa na madogo ya jinai na ya usalama barabarani. Makosa ya jinai yamegawanywa katika makundi matatu; makosa dhidi ya binadamu, makosa ya kuwania mali na makosa dhidi ya maadili ya jamii. Katika kipindi cha Januari hadi Desemba, 2019, jumla ya matukio 2, 907,333 ya jinai na usalama barabarani yaliripotiwa katika vituo vya polisi nchini yakilinganishwa na jumla ya matukio 3, 314,523 yaliyoripotiwa katika kipindi kama hicho cha mwaka 2018. Huu ni upungufu wa matukio 407,190 sawa na asilimia 12.3.

Click Here to Download the Crime Statistics Report Jan - Dec 2019 (PDF Format)

Click Here to Download the Crime Statistics Report Jan - Dec 2019 (Zip Format)