Viashiria vinavyotokana na Utafiti huu vinasaidia kutambua hatua tuliyofikia katika sekta ya afya ili kuweza kupanga mipango mbalimbali ya kitaifa na kimataifa pamoja na jamii kwa ujumla.
Utafiti wa TDHS/MIS 2021-22 unakusanya takwimu katika ngazi ya kaya kwa dhumuni la kuwezesha upatikanaji wa takwimu sahihi na zenye ubora kuhusiana na taarifa za msingi za kaya na jamii.