Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2019 umeongezeka hadi asilimia 3.5 kutoka asilimia 3.2 kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili, 2019.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2019 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili, 2019. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 117.23 mwezi Mei, 2019 kutoka 113.24 mwezi Mei, 2018.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Mei ,2019