Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2019 umepungua hadi asilimia 3.6 kutoka asilimia 3.7 kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2019.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2019 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2019.

Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 116.01 mwezi Agosti, 2019 kutoka 112.01 mwezi Agosti, 2018, sawa na  ongezeko la asilimia 3.6. Hata hivyo, kumekuwa na kasi ndogo ya mabadiliko ya bei kwa mwezi Agosti, 2019 ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo mwezi Julai, 2019.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Agosti, 2019