Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2019 umeongezeka hadi asilimia 3.8 kutoka asilimia 3.6 kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2019. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2019 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2019. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 116.39 mwezi Novemba, 2019 kutoka 112.17 mwezi Novemba, 2018.    

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Novemba, 2019