Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba, 2019 umebaki kuwa asilimia 3.8 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2019.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba, 2019 imebaki kuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2019. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 117.10 mwezi Desemba, 2019 kutoka 112.76 mwezi Desemba, 2018.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Desemba, 2019