Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2020 umepungua hadi asilimia 3.7 kutoka asilimia 3.8 kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba, 2019.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2020 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba, 2019. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 117.60 mwezi Januari, 2020 kutoka 113.38 mwezi Januari, 2019.    

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Januari 2020