Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2020 umebaki kuwa asilimia 3.7 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2020.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2020 imebaki kuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2020. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 118.92 mwezi Februari, 2020 kutoka 114.63 mwezi Februari, 2019.    

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Februari 2020