Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili, 2020 umepungua hadi asilimia 3.3 kutoka asilimia 3.4 kwa mwaka ulioishia mwezi Machi, 2020. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili, 2020 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Machi, 2020. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 120.67 mwezi Aprili, 2020 kutoka 116.82 mwezi Aprili, 2019.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Machi 2020