Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2020 umepungua hadi asilimia 3.2 kutoka asilimia 3.3 kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili, 2020.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2020 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili, 2020. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 120.93 mwezi Mei, 2020 kutoka 117.23 mwezi Mei, 2019.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Mei 2020