Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2020 umeongezeka kidogo hadi asilimia 3.3 kutoka asilimia 3.2 kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2020.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2020 imeongezeka kidogo ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2020. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 120.50 mwezi Julai, 2020 kutoka 116.61 mwezi Julai, 2019.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Julai 2020