Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2020 umebaki kuwa asilimia 3.3 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2020. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2020 imebaki kuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2020. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 119.87 mwezi Agosti, 2020 kutoka 116.01 mwezi Agosti, 2019.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Agosti 2020