Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2020 umepungua hadi asilimia 3.0 kutoka asilimia 3.1 kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2020. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2020 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2020. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 119.84 mwezi Novemba, 2020 kutoka 116.39 mwezi Novemba, 2019.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi November 2020