Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi. 

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2021 umeongezeka kutoka asilimia 3.2 kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba, 2020 hadi asilimia 3.5.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2021 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba, 2020. Fahirisi za Bei zimeongezeka kutoka 98.07 mwezi Januari, 2020 hadi 101.53 mwezi Januari, 2021.     

 

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Januari, 2021