Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2021 umebaki kuwa asilimia 3.3 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili, 2021.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2021 imebaki kuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili, 2021. Fahirisi za Bei zimeongezeka kutoka 100.85 mwezi Mei, 2020 hadi 104.22 mwezi Mei, 2021

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Mei, 2021