Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2021 umeongezeka hadi asilimia 3.6 kutoka asilimia 3.3 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2021. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2021 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2021. Fahirisi za Bei zimeongezeka kutoka 100.68 mwezi Juni, 2020 hadi 104.30 mwezi Juni, 2021

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Juni, 2021