Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia Septemba, 2021 umeongezeka kidogo hadi asilimia 4.0 kutoka asilimia 3.8 kwa mwaka ulioishia Agosti, 2021. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Septemba, 2021 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia Agosti, 2021. Fahirisi za Bei zimeongezeka kutoka 99.68 Septemba, 2020 hadi 103.71 Septemba, 2021.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Septemba,2021