Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2021 umeongezeka kidogo hadi asilimia 4.1 kutoka asilimia 4.0 kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2021. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2021 imeongezeka kidogo ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2021. Fahirisi za Bei zimeongezeka kutoka 99.93 mwezi Novemba, 2020 hadi 104.08 mwezi Novemba, 2021.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Novemba,2021